Waziri Jenista Mhagama atembelea shamba lenye ukubwa wa ekari 6000 Mvomero
Waziri Jenista Mhagama akiwa na Naibu Wake Anthony Mavunde katika ukaguzi wa shamba lenye ukubwa wa ekari 6000 ambalo ni mahsusi kwa ajili ya Ufugaji wa Ng’ombe na Mbuzi Wami Sokoine Mvomero leo tarehe 23.04.2017.
Katika eneo hilo pia kutakuwa machinjio ya mifugo na kiwanda cha kuchakata nyama ambacho kinatarajiwa kutoa Ajira zaidi ya 3000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
Pamoja na kiwanda hicho,pia kutakuwa na chuo cha mafunzo ya uchakataji wa ngozi na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na ngozi.
Wafugaji watapata soko la uhakika la mifugo yao na hivyo kutatua changamoto ya ukosefu wa masoko ya uhakika kwa wafugaji hasa katika Mkoa wa Morogoro na nchi nzima pia,jumla ya Ng’ombe 300 watachinjwa kila siku.
mjengwablog
No comments:
Post a Comment