Taasisi ya Kimichezo ya Tottenham inayomiliki miongoni mwa vitega uchumi vingi ikiwemo Timu ya Tottenham Spurs ya Jijini London, iliyowapiga Mashetani Wekundu goli 2 - 1 kwenye mechi yao ya mwisho, wamesema ushindi wao ndani ya White Hart Lane ulikuja ‘kama Baraka’ (Blessings).... endelea kusoma
|
Bango kubwa linaloutambulisha Uwanja mkuu wa Spurs wa White Hart Lane |
Taasisi ya Kimichezo ya Tottenham
inayomiliki miongoni mwa vitega uchumi vingi ikiwemo Timu ya Tottenham Spurs ya Jijini London, iliyowapiga Mashetani Wekundu goli 2 - 1 kwenye mechi yao ya mwisho, wamesema ushindi wao ndani ya White Hart Lane ulikuja ‘kama Baraka’ (Blessings) kwa ajili ya kuuaga uwanja wao na kukabidhi funguo kwa Mkandarasi aliyepewa jukumu la kuubomoa uwanja huo na kuujenga upya... amesema Mwenyekiti wa klabu hiyo, Daniel Levy huku akiandaa timu yake kwa kuhamia Uwanja wa Wimbley kwa muda msimu ujao wa Ligi.
Asubuhi ya leo blog
yako ya Matukio imeangazia pilikapilika nyingi za vifaa vya kisasa na vyenye
uwezo mkubwa zinazoendelea na bomoa bomoa hiyo iliyoanza majira ya asubuhi jana
tarehe 16/05/2017. Kazi ya ubomoaji inatarajiwa kuchukua takriban miezi mitatu
na kukamilika katikati ya mwezi September, 2017 huku maandalizi ya uwanja mpya
wenye hadhi ya ‘sports arena’ yakiwa yamepamba kasi.
Licha
ya uzee wa Uwanja huo uliojengwa mwaka 1899 lakini pia wamiliki wametoa sababu
lukuki za ujenzi wa uwanja mpya ikiwemo kudhibiti wizi wa mapato ya mlangoni,
ufinyu wa mahitaji kwa michezo mingine, na udogo wa uwanja.. wamefafanua uwanja
mpya utakuwa na uwezo wa kuchukua takriban watu 61,500 wa kukaa kwa
mkupuo, na utakuwa ‘multipurpose kwa
michezo mbalimbali ikiwemo ‘American Football’ e-Sports & Betting Center.
Mkurugenzi Mkuu wa Spurs Donna-Maria
Cullen alipoulizwa kuhusu majonzi ya kuachana na uwanja aliouzoea alijibu kwa
mkato.. ‘we are not moving anywhere, we’re overlapping” akimaanisha hawahami,
bali wanabadilisha tu mandhari ya uwanja huo uliodumu kwa miaka 118.
Alibainisha
Uwanja Mpya wa Spurs ni ‘ambitious project’ utakaogharimu pauni za kingereza zaidi ya million 800 sawa na shilingi za Kitanzania trillion 2.3; Cullen alisema uwanja mpya unatarajiwa kuwaingizia mapato kwa
watakaoukodi kwa kiasi cha pauni milioni tatu kwa kila tukio sawa na shilingi billion 8.6.
Mbali
na tenda kubwa ya miaka 5 ya mechi za NFL, uwanja mpya unatarajiwa kuwa kitovu (hub) kwa
ajili ya e-sports & betting baada ya ujenzi unaotarajiwa kukamilika msimu
wa Ligi 2019/2020.
Mechi ya mwisho ya Man U na Spurs ilihudhuriwa na mastaa
mbalimbali waliowahi kuipaisha timu hiyo kwenye kilele cha mafanikio akiwemo Ledley King, Teddy Sheringham na Staa kipenzi cha Mashabiki, David Ginola...
|
Zoezi la ubomoaji wa uwanja likiendelea kwa kasi |
|
Heavy duty Caterpillars zikiwasili kuongeza nguvu |
|
Main Gate ya kuingilia White Hart Lane |
|
Safety Signals nje ya Uwanja kuashiria shughuli za ujenzi zinazoendelea |
|
Mojawapo ya vifaa vya ubomoaji vikiwa tayari kwa shughuli hiyo. |
|
Geti la upande wa Kusini mwa Uwanja wanakoingilia mashabiki wenyeji |
|
Picha ya Juu ikionesha umati wa Mashabiki waliohudhuria mechi ya Spurs na United. |
|
Mashabiki walivyofurika uwanjani baada ya kipenga cha mwisho kuashiria kuagana na White Hart Lane |
|
Unavyoonekana Old White Hart Lane baada ya mechi ya mwisho uwanjani hapo. |
|
Wadau wakuu wa Spurs wakipita kwa huzuni nje ya Bango lenye maandishi 'White Hart Lane! |
|
Mashabiki wa Spurs wakiondoka na 'ngawira' baada ya kumalizika mechi yao na Man U. |
|
Aerial View ikionyesha ubomoaji sambamba na ujenzi wa Uwanja Mpya |
|
Aerial View ikionyesha ubomoaji sambamba na ujenzi wa Uwanja Mpya. |
|
Mandhari mpya ya White Hart Lane Sports Arena utakapokamilika 2019/2020 |
|
Stakabadhi ikionyesha kilele cha Ufanisi wa Spurs ndani ya Uwanja wao wa Nyumbani |
|
Nyota 'kipenzi cha mashabiki wa Spurs akijipongeza kwa Selfie ishara ya kuaga Uwanja |
|
Mastaa Teddy Sheringham na Ledley King nao walishuhudia mchezo wa mwisho ndani ya White Hart Lane |
|
Staa wa zamani wa Spurs Terry Venables |
ciaooo..
No comments:
Post a Comment