#Genk ya Mbwana Samatta yazidi kulisongesha !
Baada ya ukame
kumuandama, Mtanzania Mbwana Samatta ameamka baada ya kuifungia KRC Genk katika
uwanja wao wa nyumbani wa Luminus Arena walipofanikiwa kupata ushindi wa magoli
2-1 dhidi ya AS Eupen katika muendelezo wa michezo ya plya-off ya Ligi kuu ya Ubelgiji
msimu wa 2016/2017.
Magoli ya KRC
Genk yalifungwa na Jere Uronen dakika ya 18 na mtanzania huyo mwenye kipaji cha
kupachika vyavu kwa timu pinzani Mbwana Samatta aliyetumia vyema pasi ya
nahodha wake Thomas Buffel dakika ya 58.
Kwa upande wa AS
Eupen walipata goli lao la pekeekatika dakika ya 76 kupitia kwa mnigeri Henry
Onyekuru, ushindi huo umeifanya KRC Genk kuendelea kuongoza Kundi B kwa kuwa na
jumla ya point 19 ilizokusanya kwa kushinda michezo yake sita na kutoka sare
mchezo mmoja.
No comments:
Post a Comment