Kutoka Dodoma: Spika amewahoji Wabunge kuhusu pendekezo la kutoa posho ya siku moja ya kila Mbunge kama 'rambi-rambi' kwa familia zilizopoteza watoto wao Arusha... wote wasema ndiyooooooooooo!!



Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha azimio la kutoa posho ya siku moja kwa ajili ya rambirambi kwa familia zilizopoteza watoto katija ajali ya Karatu mkoani Arusha.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema huo ni ushauri aliopata kutoka kambi zote za Bunge na kuwa fedha hizo zitagawiwa sawa kwa familia hizo.
katika kupitisha kanuni ya kutenga fedha hizo Spika Ndugai aliwahoji wote na walikubali kwa kauli moja kwa kutamka neno 'ndiyooo' kuashiria kuwa wameridhia azimio hilo kwa kauli moja na kuweka pembeni 'uchama'

Wakati huo huo Mbunge mteule wa viti maalumu Chadema, Catherine Nyakao Ruge ameapishwa rasmi leo Jumatatu kuwa mbunge.
Ruge anaziba nafari ikiyoachwa na Dk Elly Macha aliyefariki dunia hivi karibuni.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search