Breaking News: Benki ya FBME 'majanga'... yatangazwa muflisi, yafutiwa leseni zote: BOT yaiweka chini ya muflisi ya Bodi ya Bima ya Amana(DIB) !!

Kuanzia tarehe 8 Mei, 2017, Benki Kuu ya Tanzania imesimamisha shughuli zote za FBME Bank Ltd, na imefuta leseni yake ya kufanya shughuli za kibenki na kuiweka chini ya ufilisi.

Aidha katika hatua hiyo BOT imeiteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia leo tarehe 8 Mei, 2017.


Hata hivyo BOT imewatoa shaka wenye amana, wadai na wadaiwa wawe wavumilivu wakati Mfilisi akiandaa utaratibu wa kushughulikia stahiki zao.

Endelea kufuatana nasi tukikuletea maelezo zaidi kuhusu hali halisi..

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search