Msimamo wa Ligi Kuu England hadi leo 08/05/2017: Ona Wenger "alivyoishika shati" Man U na kufufua matumaini ya nne bora EPL.
Washika bunduki wa Jiji la London Timu ya arsenal jana
ilichafua record ya Manchester United ya mechi 25 bila kushindwa kwa kuwalaza
mashetani wekundu hao wekundu kwa 2-0 mechi ya Ligi Kuu ya England Jumapili.
Ushindi huo uliweka hai matumaini ya Arsenal ya kumaliza
katika nafasi nne za kwanza, ingawa bado watatarajia timu nyingine zijikwae.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Granit Xhaka na Danny Welbeck
kipindi cha pili.
Licha ya kocha Jose Mourinho kuwaingiza uwanjani Marcus
Rashford na Jesse Lingard kujaribu kuokoa timu yake juhudi zake hazikufua
dafu..
Matokeo hayo yamewaacha Arsenal wenye mechi moja mkononi wakiwa
nafasi ya sita, alama mbili nyuma ya United ambao wanashikilia nafasi ya tano
na sita nyuma ya Manchester City ambao wanashikilia nafasi ya nne.
Pamoja na kufufua matumaini ya Arsenal kufuzu kwa Ligi ya
Klabu Bingwa Ulaya, ushindi huo wa Jumapili pia ulisaidia kufifisha rekodi mbaya
ya Wenger dhidi ya Mourinho ambapo kati ya mechi 15 Wenger hajawahi kuishinda
timu iliyokuwa inanolewa na Mourinho isipokuwa mechi ya Ngao ya Jamii ya mwaka
2015.
No comments:
Post a Comment