Mafuriko: Maafa makubwa ya mafuriko wilayani Lushoto..


Watu kadhaa wamenusurika kufa baada ya mawe na udongo kuporomoka na kuponda vibaya magari matatu Wilayani Lushoto, Mkoani Tanga.

Maafa hayo yametokea kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha. Watu wote waliokuwa kwenye magari hayo wamefanikiwa kutoka salama huku magari hayo yakiharibiwa vibaya.

Aidha uharibifu mkubwa wa miundombinu umejitokeza kama barabara kujaa udongo na kusababisha kukatika kwa mawasiliano katika maeneo mbali mbali wilayani humo. - Dar24







About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search