Picha 8: Kikosi cha Mauaji cha Man dhidi ya Celta Vigo leo.. Morinho asema ni Fahari kwake kutinga Champions kupitia Europa League...

KOCHA wa timu ya Manchester United, Jose Mourinho ambaye amegubikwa na kashfa ya usajili ya mchezaji wake nyota, Paul Pogba inayoshuka dimbani leo kuivaa Celta Vigo katika michuano ya Ligi ya Europa, amesema wana njia nyingi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya - Champions League lakini ya fahari kwao ni hii ya kupitia Europa hivyo watapambana kiume uwanjani na kulitwaa kombe hilo ambalo hawajawahi kufanya hivyo.

Paul Pogba
Licha ya faida ya bao moja la ugenini baada ya kuwalaza wenyeji wao Celta Vigo katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Hispania, Mourinho amejitapa kuwa wana nafasi ya ushindi na pia kutinga fainali ya michuano hiyo mikubwa ya Ulaya inayofikia kilele wiki mbili zijazo mjini Stockholm, Sweden.
"Kwa wapinzani wetu Celta Vigo hii ni mechi ya kihistoria kwao, lakini kwetu sisi hii ni mechi muhimu," alisema Mourinho na kuongeza:”aijalishi tulipata nini kabla, cha muhimu tunahitaji nini leo… Celta wana mahitaji, lakini siamini kuwa mahitaji ya Celta ni makubwa leo kuliko mahitaji yetu."
Mourinho amesema kukosa ubingwa katika michuano mikubwa kama hii hakumaanishi zaidi ila kunamaanisha timu yako si timu bora na isiyo na kiwango,.. na kuikosa michuano ya Europa msimu ujao inamaanisha Man U si timu nzuri.

 “Jambo ambalo si fahari kwangu wala kwa timu yangu wala kwa wachezaji wangu...” amewahimiza mashabiki kuiunga mkono timu ndani ya uwanja usiotabirika wa Old Trafford.
fuatilia kikosi kamili kitakachozima ndoto za Celta Vigo kusonga mbele na michuacho hii mikubwa.. 

Wayne Rooney

David De Gea

Juan Mata

Rashford

Michael Carrick

Ander Herrera

Phil Jones

Ciao…  

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search