MALIMWENGU: Mti wa ajabu ulioongea na kugomea Tinga-Tinga kwa kulia machozi eti using'olewe Jijini Mwanza !!
Tinga-tinga likiendelea na shughuli za kuung'oa mti huo uliozua gumzo mitandaoni |
Hayo ni kwa mujibu wa habari na picha zilizosambaa kwa kasi mtandaoni,.. ambazo Matukio imenasa 'heka heka' 'nguo-chanika' wananchi wa jijini Mwanza wakitaharuki na kumiminika kwa maelfu kwenda kushuhudia maajabu hayo.
"Muda huu jijini Mwanza maeneo ya Shule ya Msingi Isenga mamia ya watu Wamekusanyika kushuhudia Mti wa ajabu ulioongea!.." anapasha Yona Fares Maro.....
Tingatinga la Ujenzi wa barabara ya Airport liliufikia Mti huo ili kuukata na ndipo ukasema "Msinikate Jamani Naumia" na ndipo dereva wa Tinga tinga alipoishia kupiga Mayowe na watu kujaa, ...ingawa Baadae tinga tinga lilifanikiwa kuukata na Mizizi yake kuanza kutoa Damu kwa mujibu wa Mashuhuda.
Wazee wa kimila wa ulipokuwa mti walivyohojiwa nao hawakukosa la kusema.. "Kuhusu huu Mti ndugu zetu wenyeji wana Mengi ya kutueleza maana Muda huu kama unavyoona hapo pichani Mti umeshaondolewa na Wananchi wapo bize wanaushambulia kwa kugawana vipande eti kwamba vinawafaa katika Biashara zao na wengine wanaenda kutengeneza dawa" ilimaliza taarifa hiyo.
Wananchi wakigawana vipande mbali-mbali baada ya mti huo kukubali kuangushwa |
Maelfu ya watu wakiwa wamekusanyika kushuhudia mti unaosemekana kutoa machozi. |
Endelea kubofya www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com
Ciaaoo..
No comments:
Post a Comment