Mbowe 'apeta' kamati ya Maadili.. Halima Mdee out !!
Katika hatua
ambayo haikutegemewa,. \Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imempiga
marufuku Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam Mhe. Halima Mdee kuhudhuria vikao
vilivyobakia vya Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma. Hukumu hiyo
imekuja kufuatia ushahidi uliojitosheleza mbele ya kamati na kujiridhisha
kuwa Mhe. Mdee alidharau mamlaka ya kiti na kutoa lugha ya matusi ndani ya
ukumbi wa Bunge,
Wakati huo
huo, Kamati hiyo ya Bunge imemsamehe Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kosa la kudharau Mamlaka ya Bunge April
4, 2017.
Mbunge
mwingine ni Ester Bullaya ambaye amepewa karipio baada ya kukiri kosa lake sawa
na Mbowe.
Hata hivyo
adhabu ya Mhe. Mdee ni mapendekezo ya Kamati ambayo inasubiri baraka za Bunge
kwa utekelezaji au kusamehewa.





No comments:
Post a Comment