'Messi feki' anusuruka kuswekwa rumande !
Kijana Reza Parastesh, raia wa Iran amenusurika kutupwa mahabusu kwa kusababisha taharuki mitaani.
Reza, ambaye ni mwanafunzi, pamoja na kuwa shabiki mkubwa wa mchezaji wa Barcelona Lionel Messi, pia anafanana naye kwa muonekano. Ikiwa ni namna ya kuonyesha mapenzi yake kwa nguli wake huyo, Reza amekuwa ananyoa nywele na hata kufuga ndevu kama Messi halisi.
Bila kujiuliza kama anayepita katika mitaa ya mjini wa Hamedan uliopo magharibi ya Iran si Messi halisi, makundi ya watu walianza kumfuata Reza kila anakokwenda ili wapige naye picha hali iliyosababisha msongamano na vurugu.
No comments:
Post a Comment