'Vimodo' sasa baasi Ufaransa !!
Sheria nchini Ufaransa inayopiga marufuku
wanamitindo wembamba wasio na afya imeanza kutekelezwa.
Wanamitindo watahitajika kuwa na cheti
cha daktari kuonyesha afya yao kwa misingi ya vipimo vya uzito wao na kimo.
Wizara ya afya inasema kuwa inataka
kukabiliana na matatizo ya kutokula na viwango visivyofikiwa vya urembo.
Mswada wa awali ulikuwa umependekeza
uzito na kimo cha wanamitindo hatua iliyopingwa vikali na mashirika ya urembo
nchini Ufaransa.
Lakini aina tofati ya mswada ulioungwa
mkono na wabunge mwaka 2015 unawaruhsuas madaktari kuamua ikiwa mwamitindo ni
mwembamba mno kuambatana na uzito wake umri na mwili.
Waajiri wanaovunja sheria hiyo watapigwa
faini ya hadi dola 82,000 au kifungo cha miezi sita jela.
Ufaransa sio nchi ya kwanza kuweka sheria
inayohusu wanamitindo wembamba- Italia, Uhispania na Israel washafanya hivyo.
No comments:
Post a Comment