Neno moja tu la Mourinho baada ya Bailly kumtwanga 'mtu konde' uwanjani !
Morinho akimcheka kocha wa Vigo baada ya Mechi |
Morinho na mwanae |
NGEBE za Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho nje ya uwanja zimewahakikishia mashetani hao wekundu tiketi ya kucheza fainali ya Ligi ya Europa baada ya kutoka kifua mbele dhidi ya Celta Vigo kwa kuichapa jumla ya mabao 2-1, sambamba na kujihakikishia ushiriki wa UEFA msimu ujao.
Kwa ushindi huo,
sasa itasafiri hadi mjini Stockholm
Sweden kwenda kuumana na Ajax katika mchezo utakaochezwa Mei 24, mwaka huu na
ikitwaa itakuwa imekata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa kiulaini.
Mbali na hilo, Mourinho amesikitishwa na kitendo cha
mchezaji wake Eric Bailly kumtwangwa konde Roncaglia wa Celta na kusababisha
wote kuoneshwa kadi nyekundu.
Akijibu swali la waandishi kuhusu kitendo cha mchezaji wake kufanya
fujo hakusita kumuita Bailly mwenye kiburi na majivuno mengi – ‘a naive!!
Anasema ni kweli Man United ingeweza kutinga Ligi ya
Mabingwa Ulaya kupitia "Top Four" ya ligi ya nyumbani lakini Mourinho
alipuuzia hoja hiyo na kusema
kwake yeye 'njia rahisi ndio njia nyepesi..' na asingeweza kusubiri zaidi.
Licha ya Rooney kukaa benchi katika mechi
hiyo, aliwashukuru Rashford na Marouane Fellani kwa kazi nzuri uwanjani.
Mourinho alionekana mwenye bashasha baada ya
mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho hatua iliyoashiria wazi wapinzani wao
walikuwa na nafasi kubwa kimchezo lakini bahati haikuwa yao..
Miongoni mwa walioshuhudia mtanange wa jana
ni pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo ya United Malcom Glazer na Mtoto wa
kiume wa kocha huyo Jose Jnr aliepewa nafasi maalum jirani na benchi la Ufundi
la Man U.
Ciao… angalia picha zote za mtanange kama zilivyokusanywa blogu yako ya matukio: www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com
Konde la kwanza la Bailly |
Konde la pili likambwaga mchezaji mwenzie wa Man U |
'Hasira Hasara' hapo Bailly akilia kwa uchungu baada ya refa kumtoa uwanjani kwa kadi nyekundu |
Mkono mkono tuu.. hadi nje ya uwanja ! |
Baada ya dhiki Faraja - shujaa akilakiwa na wachezaji wenzake baada ya kuchoma nyavu za wapinzani |
'mpira si uadui guys.. acheniii.. Fellani ndivyo anavyoonekana akisema huku akiamulia.. |
hatukubali ng'ooo! wachezaji wa Vigo wakimtetea mwenzao asiendelee kupata kichapo cha Bailly |
Fellani hakamatiki baada ya kupiga bao muhimu |
Chuma kimeani... Fellani akisababisha |
Pogbaaaaa... nae alikuwepo kama kawa ! |
'masikini Rooney' ameshuhudia mechi akiwa bench ! |
No comments:
Post a Comment