Jumia Tanzania kushirikiana na kampuni kubwa kuuza simu kwa bei rahisi mtandaoni !

 Meneja wa Jumia nchini Tanzania, Hilda Kinyunyu na Marketing Manager Erick Mkomoye
JUMIA Mobile Week kuanza Mei 22 -28 ni maalumu kwaajili ya mauzo ya simu na vifaa vyake kutoka kwa makampuni makubwa Tanzania yanayoshirikiana na JUMIA. Kutakua na punguzo kubwa pamoja na zawadi mbalimbali kwa wateja watakaonunua bidhaa hizo katika website ya JUMIA.
Jumia Tanzania inashirikiana na washirika wakubwa kama Tigo na Tecno kwa mfano ili kukuletea huduma mbalimbali katika upungufu wa bei ambao watanzania wa kipato mbalimbali wanaweza kuagiza na kupata bidhaa hizo, lakini pia bidhaa za simu kutoka makampuni mbalimbali kama SAMSUNG, LG, HUAWEI pia vifaa vya simu kma headset za kusikilizia mziki zinapatikana.
Jumia mobile wiki inaanza tarehe Mei 22-28 mwezi wa tano, wateja wanaweza kuagiza simu kupitia mtandao wa jumia kwa kulogin na kuchagua bidhaa wanazotaka kisha wanajaza taarifa zao za msingi kama namba za simu na eneo wanalotaka bidhaa waletewe kisha watafikishiwa, malipo yatafanyika baada ya mteja kupata bidhaa husika na kuridhika nayo.
Kampuni ya simu ya Tecno Mobile itakua na duka maalumu katika mtandao wa Jumia ambapo simu za kampuni hiyo ikiwemo simu mpya maarufu ya Tecno Camon Cx itapatikna, pia Tecno Phantom 6, w5 na l9 plus. Mteja atakae oda simu za Tecno Mobile katika mtandao wa Jumia atapata zawadi mbalimbali zitakazomfikia pamoja na simu hiyo.
Jumia ni duka namba 1 kubwa la mtandaoni nchini Tanzania, ambapo unaweza kununua na kuuza bidhaa mbalimbali . Jumia ina bei nafuu zaidi kwa masoko ya mitandaoni kulikoa mtandao wowote nchini Tanzania, bidhaa mbalimbali zinapatikana kuanzia fashion, vifaa vya umeme, viatu, saa, michezo ya kubahatisha consoles, simu za mkononi na vidonge, Laptops na kompyuta, vipodozi na hata samani, kitu chochote unataka uwe na uhakika wa kupata mtandaoni unachotakiwa kufanya ni kuingia katika mtandao wa JUMIA.CO.TZ.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tecno Tanzania, Erick Mkomoye (kulia) akizungumzia zawadi mbalimbali mbele ya wanahabari (hawapo pichani) zitakazotolewa na kampuni hiyo kwa wateja watakaonunua simu za kampuni hiyo katika ‘Jumia mobile week’ inayotarajia kuanza Mei 22-28, 2017. Kulia ni Meneja wa Jumia nchini Tanzania, Hilda Kinyunyu.

Kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tecno Tanzania, Erick Mkomoye na Meneja wa Jumia nchini Tanzania, Hilda Kinyunyu wakionesha miongoni mwa simu kutoka kampuni ya TECNO ‘Tecno Camon Cx’ ambazo zitakuwa na punguzo la bei katika ‘Jumia mobile week’.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo.

Meneja wa Jumia nchini Tanzania, Hilda Kinyunyu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia namna ambavyo wateja watakaonunua simu kupitia mtandao wa Jumia katika ‘Jumia mobile week’ watakavyonufaika na zawadi kedekede pamoja na punguzo la bei kuanzia Mei 22-28, 2017. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Tecno Tanzania, Erick Mkomoye.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search