Picha 18: Chelsea ilivyosherehekea ubingwa wa mapema kwa style ya aina yake !

Mchezaji Michy Batshuayi alitawazwa ushujaa wa mchezo wa jana wakati Chealsea walipoilaza West Brom 1-0 katika viwanja vya Hawthorns na kujihakikishia Ubingwa wa mapema wa Ligi Kuu ya England (Premier League), hili ni goli la kwanza la Batshuayi tokea msimu huu wa ligi uanze.

Wachezaji wa chelsea wakigaragara uwanjani kufurahia ushindi
 Licha ya mechi kukosa msisimko ukionekana wazi ni mchezo wa magoli na si burudani iliyotarajiwa na mashabiki waliosafiri masafa,.. Ushindi wa jana ni mafanikio makubwa kwa kocha mdachi Antonio Conte akimaliza msimu wake wa kwanza wa ukocha ndani ya The Blues!!

Kocha Conte akiponda hoja ya mchezo mbaya uliodorora dhidi ya Broms, alisema anapima mafanikio yake klabuni kwa mapungufu ya waliomtangulia.. “..ni wazi walishindwa makocha maarufu wenye majina na kuiacha klabu ikiwa na njaa ya makombe.. na haya si mafanikio madogo kwetu” alimaliza Conte bila ya kuwataja majina ni makocha gani hasa anaowaongele...

Hata hivyo Gazeti la the mail la nchini Uingereza limebeza mafanikio ya Conte ya ushindi wa mapema na kusema chealsea si klabu ya kwanza kufanya hivyo.. usipitwe na uchambuzi wa namna watangulizi wa Chelsea walivyeweza kutawazwa ubingwa kwa miaka 10 nyuma… endelea kufungulia: www.tanzaniampyamatukio.blogspot.com

Fuatana nasi upate ladha ya Ushindi ilyofunika viunga vya jiji la London baada ya ushindi huo mwembamba wa Chelsea dhidi ya Broms…

Batshuayi akifunga goli la pekee na la ubingwa na kuwa shujaa wa mchezo 

Dieogo Costa, Terry, William na Azpill wakifurahia ubingwa

Shujaa wa mechi akipata mandhari ya uwanja baada ya ushindi

Boss Conte nae akirushwa juu na vijana wake

Terry nae akipata nafasi ya kubebwa na wenzake 

Ni zamu ya Pedro..

N'golo Kante na akapata nafasi ya kurushwa rushwa juu..

Kocha Conte akiungana na mashabiki 

Conte na Costa wakijimwagia champeni 

Furaha ikazidi kipimo wengine wakasahau hata 'bukta'


ilikuwa ni siku ya Costa kutawala furaha

kocha Conte na kaka yake Gianluca Vialli wakifurahia kombe la Premier League

Marcos Alonso, Pedro na Fabregas hawakubaki nyuma !

Goalkeeper Courtois na boss wake Conte !

Uzalendo mbele daima; ndio maneno anayosema Terry akiingia uwanjani

sherehe mpaka chumbani.

ni wakati wa ku selfika sasa.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search