Mgeni Rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na mwakilishi wa makampuni ambayo yamefadhili shughuli ya siku ya wauguzi kutoka Benki ya NMB,Suma Mwainunu.
Picha na Joel Maduka wa Maduka online.
Benki ya NMB Tawi la Geita limetoa fulana 360 kwenye siku ya Wauguzi Duniani lengo likiwa ni kuendelea na Jitihada zake za kuwa karibu na jamii.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi ambapo Kimkoa yamefanyika Mkoani Geita ,Meneja Mahusiano Biashara za serikali Kanda ya Ziwa Bi Suma Mwainunu,amesema kuwa Benk hiyo inatambua thamani ya wauguzi na kwamba ndio maana wameamua kushiriki kwa kufadhili fulana hizo.
“Tumejisikia Vizuri sana na hivyo kwa niaba ya NMB tumeweza kushiriki hafla hii kwa kutoa Shilingi Milioni Tatu ambazo zimetumika Kununua Fulana ambazo mnaona wengi Tumezivaaa wauguzi hoyeeeeee”Alisema Bi Mwainunu.
Hata hivyo Bi,Suma Ameongezea kuwa Benk ya NMB ipo karibu na wateja na ndio maana wameshiriki hafla hiyo pamoja na wateja wao.
Aidha Bi, Suma ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuiamini na kutumia Huduma ambazo zinatolewa na Benk hiyo yenye matawi mbalimbali nchi nzima na pia ametoa wito kwa uongozi wa Mkoa kushirikisha Benki ya NMB Katika maswala mbali mbali ya Kijamii nao wakiwa na uwezo wapo tayari kushirikiana nao.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa mgeni Rasmi Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ameishukuru Benki ya NMB kwa mchango wake katika kufanikisha sherehe hizo.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
|
No comments:
Post a Comment