Picha 7: Man U yajibu mapigo ya FIFA yasema 'Acha maneno, Weka Muziki.. Pogba wee mechi kwanza!!'



Licha ya sakata la FIFA na Manchester United juu ya Uhamisho wa kitita cha pauni 89.3 million za usajili wa nyota Paul Pogba, klabu hiyo imesema "ACHA MANENO, WEKA MUSIC" na kwamba Agenda kuu ya Man U kwa sasa ni mechi iliyo mbele yao usiku wa leo.

Pogba akionekana wazi kupotezea suala hilo ametinga jioni hii akiwa na timu yake katika viwanja vya mazoezi vya carrington akipasha akiwa mwenye bashasha na furaha tayari kuivaa timu ya Celta Vigo katika mchezo wao wa pili(second Leg) wa nusu fainali ya ya kombe la Europa !

Katika tangazo la FIFA lililotolewa jana Jumanne, klabu hiyo kubwa ya Jijini London imetakiwa kuweka wazi vigezo vilivyompa Mino Raiola wakala wa Pogba mgao mkubwa wa Pauni 41 million kama sehemu ya pesa ya uhamisho wa Pogba wa pauni 89.3 milion kutoka timu ya Juventus.









About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search