#SPORTPESA DEAL: Kesho ni Zamu ya Yanga !
Uongozi wa klabu ya Yanga hapo kesho unataraji kuingia mkataba na kampuni ya SportPesa kwa ajili ya kuidhamini timu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mkataba huo unatarajiwa kusainiwa makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani kuanzia mishale ya saa sita mchana.
Yanga inatarajiwa kupata udhamini mkubwa zaidi unaotofautiana na ule wa klabu ya Simba kwa mujibu wa taarifa zilizopo kutoka kwa baadhi ya viongozi na mashabiki wa klabu hiyo.
SportPesa imetoa udhamini kwa klabu ya Simba wenye thamani ya shilingi bilioni 4.9 kwa muda wa miaka mitano hivyo udhamini huo wa Yanga utakuwa ni wa pili kufanyika hapa nchini kwa klabu hizo kongwe.
No comments:
Post a Comment