Trump amtumbua alieanika barua pepe za Hillary Clinton..

Rais Donald Trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua yake ya kuliangazia swala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat Hillary Clinton, mamlaka imesema.
Ikulu ya Whitehouse iliishangaza Washington kwa kutangaza kwamba James Comey amepigwa kalamu.

Lakini wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.
Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita.
Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.
Bwana Sessions alisema kuwa idara ya haki ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika.

Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa utafutaji wa mrithi wake unaanza mara moja.
Naye kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Bwana Chuck Schumer, amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua kiongozi maalumu wa mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na Urusi.
Alisema kuwa hatua hiyo isipochukuliwa raia wa Marekani wana haki ya kuwaza kuwa Bwana Comey amefutwa ili kupunja juhudi za kukamilisha uchunguzi huo.

Ikulu ya White House imekanusha kuwa kutimuliwa kazini kwa Bwana Comey kuna uhusiano wowote na maswala ya kisiasa - bbc swahili

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search