Video: Chelsea ilipojisafishia njia UK Premier League baada ya kuibugiza Middlesbrough 3 -0
Ligi KUU ya Uingereza jana imeshika muelekeo mpya baada ya timu ya Chelsea kutoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Middlesbrough kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Wafungaji wa magoli ya Chelsea ni; Diego Costa (23'), Marcos Alonso (34') na Nemanja Matic (65') .
Kwa ushindi huo, Chelsea imezidi kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu baada ya kujikita kileleni kwa tofauti ya pointi 7 zaidi mbele ya Tottenham ambapo Chelsea wamebakiza mechi 3 kabla ya kumalizika kwa msimu huu wa 2016/17sambamba na Tottenham ambao nao wamebakiza mechi 3.
No comments:
Post a Comment