Wabunge waomba Mwongozo wajadili Mafuriko!

Wabunge wametaka shughuli za Bunge za leo ziliahirishwe ili wabunge wajadili tatizo la mafuriko liloyakumba maeneo mbalimbali nchini ambayo yameacha watu bila makazi na kusababisha vifo.


Wabunge walisimama kuomba miongozo hiyo leo asubuhi muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Walioomba miongozo ni Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani, James Mbatia (NCCR Mageuzi) na Rashid Shangazi (Mlalo-CCM).

Ngonyani maarufu kama Majimarefu ametumia kanuni ya 68(7) alisema kuwa kuna matatizo makubwa ya mafuriko nchini.

“Haswa kwenye mkoa wangu wa Tanga, kumekuwa na maafa, leo hii tunavyoongea kuna watu 1000 hawana chakula, mahali pakuishi na hawana msaada wowote lakini itawasaidiaje hawa watu wakati kamati za afya zikiendelea na utaratibu,”amesema.

Amesema watu wanaathirika na wanaweza kufa wakati wowote.

Shangazi amesema anasimama kwa kanuni 47 (1) akitaka shughuli za Bunge ziahirishwe ili wabunge wajadili kuhusu mafuriko hayo.

“Sasa hivi katika mkoa wa Tanga kuna mafuriko makubwa sana. Na jana yametokea maporomoko katika milima ya usambara, eneo la barabara Lushoto- Arusha- Mombo, Pangani kwenda Tanga, Mombo kwenda Lushoto na Kilindi kwenda Morogoro shoto zilifungwa,”amesema Shangazi.
 
Chanzo: 
Mwananchi


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search