#Zanzibar yazongwa na Mafuriko.. 'Maskuli Yafungwa' kuepusha maafa kwa wanafunzi na waalimu !

Shule zote katika kisiwa cha Zanzibar zimefungwa kwa muda kutokana na mvua kali ambayo imesababisha mafuriko.

Baadhi ya Mitaa mjini unguja ikiwa imezingirwa na maji kiasi cha kutokupitika
Waziri wa elimu katika kiswa hicho Riziki Pembe Juma amesema kuwa mvua hiyo ambayo pia imekuwa ikinyesha katika kisiwa cha Unguja na Pemba kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita pia imeharibu barabara na mali ya watu.
Alisema kuwa baadhi ya shule zimejaa maji hivyobasi kuwa vigumu kwa walimu kufunza mbali na kuwa wanafunzi wanashindwa kufika kutokana na mafuriko.
Waziri huyo amefichua kwamba uamuzi huo uliafikiwa kufuatia pendekezo kutoka kwa kamati ya kukabiliana na majanga ya Zanzibar ambayo iliishauri serikali kufunga shule hizo kwa usalama wa wanafunzi.
Baada ya kuangazia mapendekezo hayo tulikuwa hatuna njia nyengine bali kuzifunga shule hadi pale hali itakaporudia hali yake ya kawaida.
Hatahivyo amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wakifanya mitihani yao ya mwisho wataendelea kufanya hivyo.
Kufikia sasa kuna takriban wanafunzi 364 495 wa shule za msingi na zile za upili zanzibar - bbc/swahili.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search