Video: Ona Nape 'alivyojidai-dai' Bungeni, asema "tuna hatari ya kutorudi Bungeni uchaguzi ujao.."
Katika hali iliyoonekana kujifaragua katika nafasi yake ya Ubunge, Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Nnauye amekosoa vikali kipaumbele cha serikali katika kuhakikisha maji yana wafikia Wananchi Vijijini hasa wanawake ambao ndio wapiga kura wengi walioiweka serikali ya CCM madarakani.
Mbunge wa Mtama ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo hakuonyesha woga kuikosoa bajeti ya Wizara husika jambo ambalo ni tofauti na wakati alivyokuwa na kofia ya Uwaziri ambapo alikaa benchi moja na Waziri muhusika.
Nape Nnauye ameliambia Bunge kuwa katika ilani ya CCM wakati wa uchaguzi waliwaahidi wananchi kuwa watatatua changamoto za maji lakini hadi sasa bado hatua stahiki hazijachukuliwa. hivyo endapo tatizo halitoangaliwa na kutatuliwa CCM ijue wananchi hawatairudisha tena madarakani.
Full video ya mchango wa Endelea kumsikiliza nape katika video hapa chini...
No comments:
Post a Comment