Breaking News !! Anna Mghwira avuliwa Uenyekiti ACT.. #SHARE.. atakaimiwa na Yeremia Kulwa Maganja kuivusha ACT Uchaguzi wa 2018

Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo leo imefanya mabadiliko ya nafasi ya Uenyekiti wa Chama ambayo hapo awali iliyokuwa ikishikiliwa na Bi Anna Mghwira ambaye ameteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu Mpya wa Mkoa Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyopatikana mchana huu, kamati imemteua Yeremia Kulwa Maganja kukaimu nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi akisoma maazimio ya kikao kwa wandishi wa Habari
Licha ya hapo awali kuripotiwa akisema kwamba angeliendelea na uwenyekiti wa chama chake cha ACT-Wazalendo hata baada ya kuapishwa kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro, kwa mazingira ya sasa ya kazi ya Bi Anna Elisha Mghwira imeonekana wazi hataweza kuhimili nafasi mbili hizo kwa wakati mmoja. 
Hata hivyo Kamati ya Uongozi ya chama hicho iliyokutana leo jijini Dar es Salaam, imembakishia Bi Mghwira uwanachama wake wake wa kawaida wa ACT Wazalendo, 
Huku ikimpongeza Rais John Magufuli kwa kuona kuwa ndani ya chama chao muna watu wanaoweza kumsaidia kuongoza nchi, kamati imemuomba Rais Magufuli kushauriana kwanza na uongozi wa chama husika, endapo katika siku zijazo atahitajia kuteuwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani kuingia Serikalini.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search