Breaking News!!! 'Kimenuka EWURA' Waziri Mkuu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu ni Sakata lake na LHRC kuhusu IPTL.. #SHARE


Usiku wa saa saba na dakika moja kuamkia tarehe 11 June 2017 imetoka taarifa kutoka IKULU Dar es salaam ikiwa na taarifa ya maamuzi mapya ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba Waziri Mkuu Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURAFelix Ngamlagosi kuanzia leo tarehe 11 Juni, 2017.
Maamuzi haya yamekuja siku mbili baada ya habari za kampuni ya IPTL kuongezewa mkataba wa uzalishaji umeme ambapo pia Kituo cha sheria na haki za Binadamu kilijitokeza na kusema hakikubaliani na mkataba huo kuongezwa kwani kampuni hiyo inahusishwa na kashfa ya uchotwaji wa Mabilioni kupitia account ya ESCROW.
Hata hivyo baada ya kituo hicho cha LHRC kujitokeza kuongea, EWURA walijitokeza na kusema ‘kuna vitu viwili vya kuzingatia hapa, EWURA tunachodili nacho sasa hivi ni leseni ya IPTL ambayo aliipata 1996 ikiwa ni ya miaka 21 na inaisha July 2017
Sheria iliyoanzisha EWURA na sheria ya UMEME zinataka mtu yeyote anavyoomba leseni EWURA itoe taarifa kwa umma ili watu watoe maoni au pingamizi, hicho ndicho tulichokifanya na hatuendi kwa siri…. tumetoa siku 21 za kupokea maoni, kinachotendeka hapa ni IPTL kutaka kuomba kuongeza leseni‘ 
TAARIFA hii imekujia kwa hisani ya millardayo, itakumbukwa kuwa blog yako ya matukio imekuwa ikikuletea sakata hili tokea juzi ikiwemo ya jana ya EWURA 'kuipa mgongo LHRC'

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search