Good news!! Bandari ya Dar es Salaam ndani ya Upanuzi mkubwa #Share. tayari madocument yamesainiwa leo!!


Dar Es Salaam. Serikali na kampuni ya China Harbour Constructions Engineering wamesaini mkataba wa upanuzi wa kina cha mlango wa bandari ya Dar es Salaam na katika geti namba moja hadi namba saba kwaajili ya kuboresha na kupanua huduma zinazotolewa.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa ameshuhudia utiaji saini wa mradi huo ambao umesainiwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya bandari (TPA), Deusdedith Kakoko kwa upande wa Serikali.
Akiuzungumzia mradi huo Waziri Mbarawa alisema gharama ya mradi ni Sh 336 bilioni na utatekelezwa kwa miezi 36 lakini Serikali inaendelea na mazungumzo na kampuni hiyo iliyopewa tenda ili kupunguza bei na kakamilisha mapema kabla ya muda huo uliokadiliwa awali.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search