EWURA 'waipa mgongo LHRC' kuhusu IPTL, #SHARE, awataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni !!

Licha ya msimamo mkali wa Kamisheni ya Sheria na Haki za Binaadam(LHRC) na tahadhari kwa EWURA kutoitisha maoni ya kuipa mkataba IPTL hadi watoe majibu kwa maswali husika,.. Mamlaka hiyo ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini, imeendelea kuwataka wananchi kuwa wazalendo kwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni kuhusu dhamira ya kampuni hiyo kongwe ya kufua umeme, kuomba kuongezewa muda wa leseni yake ya kuiuzia Tanesco umeme.

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo amesema kuna baadhi ya watu wanapotosha umma kwamba tayari IPTL wameshapewa leseni ya kuiuzia umeme Tanesco.

"Ewura tunapokea maoni ya wananchi kwa maandishi, kwa hiyo itakuwa ni jambo la kizalendo kwa wananchi kujitokeza na kutoa maoni ama kupinga IPTL au kuunga mkono ili itusaidie nasi kufanya uamuzi," amesema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Ewura, Edwin Kidifu amesema mchakato unaofanyika sasa ni wa kisheria na maoni ya wadau ndiyo yataamua IPTL ipewe leseni au laa!

Kidifu anasema IPTL imeomba kuongezewa muda wa leseni yake kwa sababu mkataba wake wa miaka 20 na serikali wa utekelezaji wa mradi wa umeme unakwisha mwaka 2022.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search