BUNGE la EALA matatani, Wabunge wapya hawataapishwa mpaka majibu yapatikane kwa maswali haya.. #SHARE


Bunge la Afrika Mashariki(Eala) lililochaguliwa hivi karibuni, limeingia matatani baada ya mwananchi mmoja raia wa nchi ya Sudani Kusini kufungua kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki(EACJ)kupinga utaratibu uliotumika kuwapata wabunge tisa(9) kutoka Jamhuri ya Sudan ambayo inajumuisha pande mbili.

Hatua hiyo ya kuweka pingamizi inazuia shughuli zote za Eala ikiwamo kuwaapisha wabunge wapya wa bunge la nne hadi ufumbuzi wa suala la nchi yake yake utakapotolewa uamuzi na mahakama hiyo.

Hata hivyo shughuli za kuwaapisha wabunge zilizokuwa zifanyike Juni 5 hazikufanyika kutokana nchi ya Kenya kutokukamilisha taratibu za uchaguzi wa wabunge wa nchi watakaoiwakilisha Eala.

Kenya imeshindwa kuwachagua wabunge wa Eala kutokana harakati za uchaguzi Mkuu  zinazoendelea nchini humo hatua iliyoyumbisha akidi katika bunge la tatu lililomaliza vikao vyake wiki iliyopita jijini Arusha. 

Na Mwandishi wetu.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search