Hisia mchanganyiko.. Watanzania wakiadhimisha siku ya Uchangiaji Damu Duniani.. #share
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wameitikia wito na kujongea katika vituo mbalimbali kwa ajili ya kuchangia damu ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuchangia damu.
(Picha mbili juu baadhi ya Wasamaria wakijitolea damu)
Mmoja wa wachangiaji hao ambae alitambulika kwa jina moja tu la Hamza alisema ameguswa kutoa damu yake ili kuokoa maisha ya wengine wenye uhitaji.
"Sina uwezo wa fedha lakini damu ninayo nimeona nami nitoe mchango wangu kuokoa maisha ya wengi ambao wako hospitalini wanaihataji tiba hii muhimu isiyopatikana mahali popote zaidi ya kwa binadamu," alimalizia mchangiaji huyo..
No comments:
Post a Comment