U-Heard.. Dar es Salaam pamefanyika makosa 404,571 ya kiusalama barabarani kwa kupindi cha January hadi May, 2017.. #share

Imeelezwa kwamba makusanyo ya tozo mbalimbali ya makosa ya usalama barabarani kwa mkoa wa Dar es Salaam yameongezeka kutoka Sh7.3 bilioni hadi Sh12.8 bilioni.

Ongezeko hilo linatokana na makusanyo yaliyofanyika kuanzia January mpaka May mwaka jana na Januari hadi Mei mwaka huu.


Hayo yamesemwa leo asubuhi na Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya katika halfa ya kukabithi jumla ya magari 26 ya doria kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya mtengenezo.

Alisema kiwango hicho cha faini ni kutokana na ongezeka la  makosa ya usalama barabarani kutoka kiwango cha jumla ya  makosa 404,571 katika kipindi cha kuanzia January mpaka  May mwaka huu, kutoka jumla ya makosa 246,695  kwa kipindi sawa na hicho mwaka jana.

Pia, katika kipindi cha kuanzia January hadi May mwaka, huu jumla ya kesi 1723 za makosa ya usalama barabarani zilipelekwa mahakamani, kutoka jumla ya kesi 1135 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la kesi 588 sawa na asilimia 34.

“Ongezeko la makosa ya usalama barabarani ni kutokana na mji kukua kwa kasi na idadi ya watu kuongezeka... jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani litaendelea kusimamia sheria na kutaka madereva watiii sheria bila shuruti,”

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search