JUVE VS MADRID au ZIDANE VS RONALDO ?? Zidane amaliza utata #SHARE halafu endelea..

Zidane 'avua kofia kwa Ronaldo' akiri hakuwahi kufikia nusu ya 'mpira wa Cristiano'!!


Katika hali isiyotarajiwa, na masaa kadhaa tu kabla ya fainali ya UEFA CHAMPIONSHIP fainali, kocha mkuu Real Madrid inayokutana na vikongwe Juventus..  'Ze Soccer Galancha' Zinadine Zidane ameweka 'unazi' pembeni na kummwagia sifa kibao nyota wake tegemewa Cristian Ronaldo, akipasua wazi kuwa katika zama zake za kusukuma 'ndinga' hakuwahi kufikia hata nusu ya ubora wa kijana wake huyo uwanjani !

Ronaldo nae ambae anaesifika kwa 'Golden ha trick' amesema hawezi kuwa mnafiki.. na kurudisha heshima kwa boss wake, akikiri bila kocha, mchezaji peke yake si chochote si lolote uwanjani.." 

Huku macho na masikio yakielekea Cardiff kushudia Zidane akiiandikia Madrid Zedane akivunja mwiko na kulibakisha kombe kwa msimu wa pili mfululizo, jambo ambalo hutokea kwa nadra sana, na Juventus nao wakitaka kukomaa kukamata kombe hilo ambali wamelisotea kwa mda mrefu na kuambulia kuwa wasindikizaji tuu !!!

Hebu msomaji dondosha maoni hapo chini nani zaidi;... Zidane au Cristiano ?





About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search