Neno la Zari baada ya kuzagaa habari kuhusu Mahakama 'kutengua ' mazishi ya mumewe wa zamani!!
Siku ya jana Ijumaa ya tarehe 2 June, Mahakama nchini Uganda iliandika historia baada ya kutoa 'warranta' ya kutengua mazishi ya kifahari aliyofanyiwa Ivan Ssemwanga a.k.a Ze Don Ivan' ambaye pia aliwahi kuwa mume na mzazi mwenziwe na Zari ambaye kwa 'sasa ni mchumba'wa Diamond Platnumz mwanamuziki Staa wa Bongo Fleva wa Nchini Tanzania.
Kabla ya Utenguzi huo wa Mahakama, Zari alilisifia sana kundi la 'The Rich Gang' kwa hatua ya kumtunza na kumuenzi Ivan na kukiita cha kumwagia fedha badala ya mashada ya maua ni cha "kiungwana na ni muhimu katika kukumbuka fadhila aliyowafanyia Waganda wakati wa Uhai wake..."
Hata hivyo, tokea jana baada ya hatua hiyo ya mahakama, Zari amekuwa kimya kama 'maji ya mtungi' wanyetishaji wakidai anatafakari 'cha kuzifanyia pesa hizo...'
Matukio bado inafuatlia kuona kama 'maelfu hayo ya mshiko' yakifukuliwa atakubali yaingie kwenye mzunguko au atasema ni mali ya watoto wake?
No comments:
Post a Comment