DC Mjema aadhimisha Siku ya Mazingira Kimkoa; aelezea Changamoto za Taka Viwandani!!


Shughuli za viwanda jijini hapa zimetajwa kama chanzo cha kuzalisha taka ambazo asilimia 50 hupelekwa katika maeneo ya kutupia taka na asilimia 50 hubaki mtaani.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema hayo kwenye maadhimisho ya siku Mazingira Duniani ambayo kimkoa yaliyafanyia Wilaya ya Ilala.
Mjema alisema jiji hili lina viwanda vikubwa na vidogo takribani 1,885 ambavyo huzalisha taka tani zaidi ya 4,500 kwa siku.
"Takribani asilimia 50 ya taka zinazozalishwa huzolewa na kupelekwa kwenye kituo cha taka, lakini asilimia 50 hubaki mtaani," amesema Mjema.
Mjema alisema changamoto huyo husababishwa na uwezo mdogo wa Halmshauri.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search