Muhimbili yaandika historia ya tiba nchini.. yapandikiza vifaa vya usikivu kwa wagonjwa wanne, ni ya kwanza ya kipekee Nchini !!

Kwa mara ya kwanza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imefanikiwa kupandikiza vifaa vya  usikivu kwa wagonjwa wanne, ikiwa ni mara ya kwanza upasuaji wa aina kufanyika nchini. 

Hatua hiyo inaelezwa kuwa inaiwezesha Tanzania kuwa nchi ya pili barani Afrika ikiifuatia Kenya kufanya upasuaji huo, ambao unawezesha kuzinduliwa kwa huduma hiyo nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua huduma ya upasuaji na upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watoto waliozaliwa na tatizo hilo.

"Haya ni mafanikio makubwa kwa Serikali kwani licha ya kuwesha wananchi wengi wenye tatizo hilo kuhudumiwa, pia inapunguza gharama ambazo tumekuwa tukitoa ili kugharamia upasuaji huu," alisema.

Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Mseru alisema mwaka jana Serikali iligharamia matibabu ya wananchi 50 waliokuwa na matatizo hayo. 
"Matibabu ya matatizo haya yanatibiwa kwa gharama kubwa mgonjwa mmoja upasuaji wake unagharimu kati ya shilingi 80 milioni hadi shilingi 100 milioni,"alisema Profesa Mseru. 

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search