Neno la Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi Baada ya Taarifa za Maalim kuhamia Ofisi Mpya za kisasa - Magomeni !!
“Naamini Chama cha CUF kitafanya mambo yake kwa mujibu wa kuzingatia sharia zinazoongoza mwenendo wa Vyama vya Siasa Nchini…”
![]() |
Taswira ya Jengo jipya na la kisasa zilipo Ofisi kuu za Chama cha CUF |
Hayo ni maneno
ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akitoa ‘neno’ baada ya kuzagaa
kwa taarifa za Maalim Seif kufungua na kuendesha ofisi za chama hicho maeneo ya
Mtaa wa Idrissa mjini Magomeni Mapipa – Jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Jaji Mutungi amesema hajapata taarifa yoyote rasmi
ya chama hicho juu ya kufungua ofisi mpya mbali na kuyasikia kupikia vyombo vya
habari.
"Ukiondoa taarifa za
kwenye media sijapata taarifa yoyote kutoka CUF labda wawe wameleta leo (jana),
lakini naamini chochote wanachofanya wanaelewa taratibu wataleta
taarifa,”amesema Jaji Mutungi.... Msajili amesema sheria inawataka wanapofungua ofisi watoe
taarifa ndani ya siku 14, ambazo hazijaisha hivyo anaamini wanajua hilo.
Kwa mujibu wa taarifa zinazoendelea kusikika, Upande wa
Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad uamefungua ofisi hizo, baada ya tukio la
kuvamiwa katika Ofisi Kuu za Buguruni na kundi linalotambulika na ofisi ya
Msajili la Profesa Ibrahim Lipumba.
Jaji Mutungi amesema atakapopokea taarifa rasmi ataangalia
kama taratibu zikifuatwa kwani ufunguaji wa ofisi mpya una taratibu zake.
“Nikiletewa taarifa ndio nitajua kama walifata taratibu au la, ufunguaji wa
ofisi una taratibu zake najua wanazijua pia,” alimalizia Jaji Mutungi.- masaa 24
No comments:
Post a Comment