News 10: China Yasalimu Amri, Yakabidhi Mamlaka ya Hong Kong Baada ya Miaka 20 ya Kuikalia.. #share.. "WALETENI huku wanafunzi waliojifungua wapate Elimu.. !"

HONG KONG- LICHA ya harakati mbalimbali za kudai uhuru kamili wa Hong Kong kutoka China, Rais Xi Jinping amewasili mjini hapa ili kuadhimisha miaka 20 tangu China ilipokabidhiwa utawala kamili juu ya Hong Kong.


Akizungumza mbele ya halaiki iliyojitokeza uwanja wa ndege kumlaki, Rais Jinping alisema kwamba; “Baada ya miaka 9, hatimaye tena naikanyaga ardhi ya Hong Kong. Ninajisikia furaha isiyo na kifani, kwani Hong Kong imekuwa na sehemu kwenye moyo wangu muda wote.”

Hata hivyo, ujio wa Rais Jinping mjini hapa haukufurahiwa na watu wote kwani kabla ya ujio huo mamia ya wanaharakati na waandamanaji ambao wamekuwa wakidai uhuru kamili wa Hong Kong wamekamatwa na kuwekwa ndani ili wasivuruge sherehe hizo zinazotarajiwa kufanyika Jumamosi.

Miaka 20 iliyopita, utawala wa Uingereza uliirudisha Hong Kong katika mikono ya China chini ya mfumo ujulikanao kama ‘Taifa moja, Mifumo miwili’ ambao unaipa mamlaka China ya kuitawala Hong Kong kiuchumi na kiutawala.
SkyNews








About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search