News! Mbunge Kishoa ataka benki ya Stanbic ifutiliwe mbali!! #share

Mbunge wa Viti Maalum Bi Jesca Kishoa, ameitaka Serikali Kuifunga Benki ya Stanbinc kama iliyofanya kwa Benki ya FBME.


Mhe. Kishoa amesema, Benki ya Stanbic inastahili kufutwa kwa kuhusika kwake kwenye miamala iliyothibitika kuhusisha rushwa huku akivilaumu vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutochukua hatua kwa wakati.

"Uamuzi wa kuifuta Benki ya FBME ulitokana na uchunguzi uliofanywa na mamlaka za nchini Marekani wakati tunavyo vyombo vya uchunguzi nchini. Vinafanya nini?" amehoji Jesca.

Wakati akiitaka Serikali kuchukua hatua hiyo amehimiza vyombo vya uchunguzi kujielekeza kwenye masuala makubwa ya kutaifa ili visionekane vinawashughulikia wapinzani.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search