Ewe Mtanzania.. Ni haki yako kuzifahamu Nchi hizi 80 ambazo unaweza kuzitembelea bila kuhitaji VIZA..#share

Serikali imesema kuna zaidi ya nchi 80 ambazo Watanzania wanaweza kuzitembelea bila kuhitaji viza.

Hilo limeelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, Rashid Shangazi aliyetaka kuzifahamu.

"Zipo nchi 16 Afrika na 67 duniani ambazo Watanzania wanaweza kuzitembelea bila kuwa na viza," amesema Masauni

Licha ya nchi za Afrika Mashariki, alizitaja Benin, Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Coast, Djibouti, Gabon, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Sierra Leone na Togo ambazo hutumia mfumo wa visa on arrival.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search