Pichani: IGP Sirro atembelea kijijini Mangwi alikouawa Mwenyekiti,.. #share atoa pole kwa wafiwa...

Siku moja baada ya kuripotiwa mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, IGP Simon Sirro ametembelea kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa.
Aidha, IGP Sirro amewataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo akiwataka kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.

IGP Simon Sirro akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mangwi, Kata ya Mchukwi alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji.

IGP Sirro aizungumza na Wananchi wa Mangwi alipowatembelea baada ya mauaji ya Mwenyekiti wa Kijiji na Afisa Mtendaji

IGP Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa Wananchi wa kijiji cha Mangwi

IGP Sirro akikagua nyumba iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi. (Picha zote na Hassan Mndeme – Jeshi la Polisi).

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search