Tashwishi yapanda, Lowasa akiwasili kuhojiwa Ofisi ya DCI,..#share.. Ulinzi umeimarishwa Barabara ya Ohio !

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mwanachama wa Chama cha Chadema Edward Lowassa amewasili katika afisi ya mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai baada ya kutakiwa kufika katika afisi hiyo siku ya Jumatatu kwa sababu zisizojulikana .
Kulingana na shirika la Utangazaji la BBC, Bwana Lowassa ambaye alitakiwa kuwasili katika afisi ya DCI muda wa saa nne aliwasili saa tatu na dakika 58 asubuhi.
Msafara wake ulikuwa na magari sita ikiwemo magari mawaili ya polisi yaliokuwa na na polisi waliojihami .
Taarifa zinasema kulikuwa na ulinzi mkali maeneo ya jirani, na mashuhuda wanasema hakukuwa na 'pisha-pisha' nyingi mtaa wa ohio kama ilivyo kawaida ya mtaa huo maarufu Jijini Dar es Salaam na Waandishi habari walikatazwa kuchukua picha za bwana Lowassa.
Katika mahojiano ya simu na gazeti la The Citizen, alisema kuwa anashuku kwamba agizo hilo la kutakiwa kujiwasilisha linatokana na matamshi aliyotoa mjini Dar es salaam siku ya Ijumaa wakati wa hotuba ya Iftar, ambapo pamoja na mambo mengine alimtaka Rais magufuli kuwaachilia huru wahubiri wa Kiislamu ambao walikuwa wamekamatwa kwa zaidi ya miaka minne bila kesi zao kuamuliwa. - BBC swahili


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search