Tibaijuka ang'aka Bungeni,.. adai na yeye ni 'mhanga wa Tetemeko!! #share.
Dodoma. Aliyekuwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ameitaka Serikali kuwapa kipaumbele waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mwaka jana.
"Wahanga wa tetemeko hatujioni kwenye bajeti hii. Sijaona mpango wa kuwatunza walioathirika na tetemeko lililotokea. Naomba viwanda hasa vya ujenzi vifungue outlets (matawi) ili kuwawezesha wananchi kujenga makazi mapya," amesema mbunge huyo wa Muleba Kusini.
Ameyasema hayo leo wakati aichangia mpango wa bajeti ya Serikali unaoendelea bungeni hapa.
Tetemeko la ardhi mkoani humo lilitokea Septemba 10 mwaka Jana na kusababisha maafa ikiwamo uharibifu wa miundombinu ya barabara na majengo pamoja vifo na majeruhi kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment