Top 10 News: Waziri Mbarawa 'amuweka mtu kati' Mkandarasi wa maegesho ya kivuko,.. #share Dada wa Mombasa amfungia safari Ali Kiba,.. CCM imeridhishwa na kasi ya JPM..

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa MAKAME MBARAWA, amemtaka mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa maegesho kwa ajili ya kivuko kuhakikisha maegesho hayo yanakuwa imara ili yadumu kwa muda mrefu.




Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukagua maegesho hayo, Waziri MBARAWA, pamoja na kumtaka mkandarasi huyo kujenga miundombini bora na kudumu, pia amemtaka kuharakisha ujenzi huo ambao hadi kukamilika kwake utagharimu Shilingi BILIONI 1 na Milioni 9 00 .

Ujenzi wa eneo la maegesho unatarajia kukamilika  Novemba mwaka huu na kwamba kukamilika kwa ujenzi huo na kuletwa kwa kivuko kutasaidia wananchi wa Lindi Mjini na Lindi Vijijini kupata usafiri wa uhakika na salama zaidi  - Source ITV








About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search