Video: ANNA Mghwira Afunguka kuhusu majukumu yake mapya.. "nimesema sio tena mtu ananifuata Ofisini kwangu kuniulizia mambo ya ACT!!

Mkuu mpya wa mkoa Kilimanjaro Anna Mgwira, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu mustakbali wake wa kisiasa baada ya kupewa majukumu hayo mapya ya kulitumikia taifa kupitia ukuu wa mkoa huo.

Katika mahojiano maalum, Bi Mgwira amefunguka kuwa ana nia na uwezo wa kutimiza majukumu yake mawili kwa vile hayana muingiliano wala ukinzani wowote.. amebainisha kuwa siku za kazi atakuwa ofisi ya umma, na mwishoni mwa wiki atazitumia kwenye majukumu ya chama chake kama Mwenyekiti kwa kutumia rasilimali zake binafsi kama vyombo vya usafiri. 

Mwisho kabisa ametahadharisha wanachama na wadau wengine wa chama kutomfuata ofisini kwake kumuuliza mambo ya ACT Wazalendo kuepusha muingiliano wa majukumu.

Msikilize mama Mghwira kwenye video hii fupi.



Hapo Awali:
Licha ya mijadala inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii ya kuvuliwa au kutovuliwa Uenyekiti wa ACT wazalendo, Mkuu mpya wa Mkoa kilimanjaro Bi Anna Elisha Mghwira, leo aliwasili mapema katika kituo chake cha kazi kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake Mapya kufuatia kuapishwa kwake na Rais JPM juzi Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

Akiwa mwenye uso wa furaha, bashasha tele na kujiamini, Bi Mghwira alionekana akisani kitabu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa mkoa kuashiria ujio mpya wa ugeni katika ofisi hiyo..

Matukio blog tumenasa picha ya tukio zima la Mkuu huyu mpya akiwa ndani ya ofisi yake mpya mara baada ya kuwasili ofisin hapo leo asubuhi.. #SHARE

endelea kufuatana nasi kupitia kiunganishi chako: www.matukiotza.blogspot.com 

Pia kama ulipitwa na hii video akiwa nyumbani kwake..play 



About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search