Top news: Serikali Yaongeza Wiki mbili Kodi ya Majengo.. #share Ewura "yashusha neema" kwa wenye Magari.. ni kuanzia 01/07/2017

Mamlaka ya Mapato (TRA) nchini imeongeza siku 14 za ulipaji wa kodi ya majengo ili kuwasaidia wale ambao wamechelewa kukamilisha mchakato huo.


Hayo yameelezwa leo Ijumaa (Juni 30) na Meneja wa TRA, Temeke, Warioba Kenere, ikiwa ni siku ya mwisho iliyotangazwa na mamlaka hiyo kwa wananchi kulipa kodi ya majengo.


Ni jana Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi wa TRA wa Richard kayombo alitahadharisha kuwa hawataongeza muda wa kulipa kodi hizo na badala yake ambao hawatalipa kufikia tarehe ya mwisho iliyowekwa watatakiwa kulipa faini ya Sh 75,000.









MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei kikomo   za mafuta ambapo petroli, diseli na mafuta ya taa yamepungua kwa sh. 37 kwa lita sawa na asilimia 1.81 huku mkoa wa Tanga bei ikipanda.

Aidha, Ewura imesema kushuka kwa bei kutasababisha bei ya petroli kuwa sh.2014 , dizeli sh.1874 na mafuta ya taa sh. 1806.

Akizungumza jana na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Ewura, Godwin Samwel alisema bei hizo zitaanza kutumika Julai mosi mwaka huu na kwamba kupungua huko kumetokana na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji mafuta.

Alisema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote ikiwa ni petroli, dizeli na mafuta ya taa zimepungua ikilinganishwa na tolea lililopita la Juni 7 ambapo kwa mwezi utakao anza wa saba bei za rejareja dizeli na mafuta ya taa zimepungua kwa asilimia 1.81

Hata hivyo alieleza kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita bei za jumla za petroli, dizeli na mafuta ya taa nazo zimepungua kwa asilimia 1.92 hii ni kwa lita 37 ambapo  lita 13 ni asilimia 0.77 na lita 18 ambayo ni sawa na asilimia 1.10.

Aidha bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli zimeongezeka kwa Mkoa wa Tanga ilikilinganishwa na toleo lililopita ambapo ongezeko hilo limetokana na mabadiliko ya soko la mafuta katika soko la dunia.

"Kutokana na kutopokea mzigo mpya wa mafuta ya taa katika Bandari ya Tanga kwa mwezi Juni mwaka huu wamiliki wa vituo vya mafuta Mkoa wa Tanga wanashauriwa kununua mafuta hayo kutoka Dar es Salaam" alisema 

Alisema katika Bunge la bajeti lilanaloendelea Dodoma lilipitisha muswada wa mabadiliko ya ushuru kwa bidhaa za mafuta ya petroli dizeli na mafuta ya taa ambapo shilingi 40 kwa lita moja zimeongezwa kwenye viwango vya awali vya ushuru.

"Kwa mujibu wa sheria ya mafuta ya mwaka 2015, bei za bidhaa  za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko na tutaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta" alisema.

Aidha alisema vituo vyote mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za mafuta katika mabango yanayoonekana na kuonesha bei ya mafuta, punguzo, kwenye vivutio vya bioashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

Hata hivyo alisema wanunuzi wametakiwa wahahakishe wanapata stakabadhi ya ,alipo inayoonesha jina la kituo ,tarehe na aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwea kil alita ambapo itatumika kama kidhibiti cha manunuzi.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search