Wadau wa Habari waililia Mawio #share

Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Umoja wa vilabu vya Habari Tanzania (UTPC) wamelaani vikali kitendo cha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe kulifungia gazeti la Mawio na kuliweka katika mzunguko kwa miaka miwili.


Tamko hilo limetolewa jana (jumapili) baada ya gazeti hilo kufungiwa juni 15 huku Waziri huyo alitumia sheria mpya ya huduma ya vyombo vya Habari ya 2016 kwa makosa ya kukiuka vifungu hivyo na agizo la Rais kutowahusisha Marais wastaafu na sakata la uporaji wa rasilimali madini.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Ole Ngurumwa amesema hii sio mara ya kwanza katika magazeti na vyombo vya Habari kufungiwa na Waziri katika nchi yetu kwa kutumia sheria mbalimbali kandamizi hasa sheria ya magazeti ya 1976 iliyofutwa mwaka 2016 na kuridhiwa na sheria ya huduma za vyombo vya Habari.

"tunapinga utaratibu wa kisheria wa kumpa waziri mamlaka makubwa katika sekta ya habari, sheria iliyopita haina tofauti na ya sasa ya kumpa mamlaka waziri kujifungia gazeti pekee na kwa makosa atakayoyaona yeye ni kinyume na maslahi ya umma, "amesema Ole Ngurumwa.

Magazeti kadhaa yalifungiwa katika siku za nyuma ikiwemo Mwananchi, Mawio, Mwanahalisi na Mtanzania.

About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search