AGIZO: JPM atoa siku 14 wamiliki vituo vya mafuta kufunga mashine za EFDs, watakao kaidi kufutiwa leseni ya biashara...# share
Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta
nchini, kuhakikisha wanaweka na kutumia mashine za kielektroniki (EFDs) na
atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo atafutiwa
leseni ya biashara.
Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi leo katika ufunguzi wa
barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154.
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais Magufuli wakati akiweka jiwe
la msingi katika ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye
urefu wa Kilometa 154.
Aidha amewataka Mawaziri wenye dhamana kuhakikisha
wanafuatilia agizo halo kuanzia sasa ili
litekelezwe kikamilifu.
"Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya
hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa
kodi", amesema
Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepiga marufuku
wananchi kutozwa kodi kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka
wilaya moja kwenda nyingine.
Rais Magufuli ameanza ziara ya siku mbili katika Mkoa wa
Kagera ambako mbali na kuongea na Wananchi, na kufungua miradi ya maendeleo ambapo
amenza kwa uzinduzi wa jiwe la msingi katika barabara ya
Kagoma-Biharamulo-Rusaunga yenye urefu wa kilomita 154 iliyojengwa kwa kiwango
cha lami ambayo imegharimu sh. bilioni 190.4.
Anatarajia katika ziara hiyo pia kufika katika mikoa ya Kigoma,
Tabora na Singida ambako atafungua na kuzindua miradi 9 kati ya Julai 19 hadi
25.
Na Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment