NEWS: Waziri Ummy amekuja na kauli hii kukabili changamoto kwa watoto wa kike shuleni....# share
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Ummy Mwalimu amewasa watoto wa kike wa shule mbalimbali nchini kutafakari matokeo ya mwaka huu ili
kuwa chachu ya kujitambua na kujikinga na mimba shuleni.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
Ummy katika tarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini cha wizara hiyo yenye lengo la kuwapongeza watoto wa kike kwa ufaulu
mzuri katika mtihani wa kidato cha sita mwaka huu.
Amesema kama wanafunzi wa kike watajitambua watasoma kwa ari kubwa kwa manufaa yao na Taifa
kwa ujumla.
Aidha taarifa hiyo imebainisha kuwa Ummy amempongeza
Sophia Juma wa shule ya Sekondari Mazinde juu (Tanga) kwa kushika nafasi ya
kwanza pamoja na Agatha Ninga wa shule ya Wasichana Tabora ambaye ameshika
nafasi ya pili kitaifa.
Kwa mujibu wa tarifa hiyo pia amewapongeza
wanafunzi wote wa kwa jitihada walizoonesha na kuweza
kufaulu mitihani yao kwa kiwango cha asilimia 97.21 ya waliofanya mtihani, ikilinganishwa
na asilimia 95.34 ya wavulana waliofaulu.
Waziri ameeleza kufarijika na
juhudi ya wanafunzi wa kike, kufuatia
ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu na kupanda kwa asilimia 94.07 katika madaraja haya
ikilinganishwa na wavulana waliofaulu kwa asilimia 93.49.
Amebainisha kwa kusema kuwa juhudi hizo sio za kubezwa ambapo alisema
kwamba ni ishara thabiti kuwa mtoto wa kike akipewa nafasi anaweza.
Amesema wizara inatambua
ushirikiano wa walimu, wazazi, na jamii ambao wamewezesha kufikiwa kwa ubora wa
ufaulu wa watoto wa Kike ambapo alibainisha kuwa juhudi zao ndizo ambazo
zimesaidia utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa fursa sawa
kwa watoto wa kike na wa kiume katika kupata haki ya elimu.
Ametoa rai kwa watoto hao wakike waelewe
kuwa wamehitimu daraja moja, hata hivyo bado wanalojukumu la kujiendeleza zaidi
katika taaluma mbalimbali kama njia ya kumwezesha mtoto wa kike na mwanamke kuchangia katika maendeleo ya taifa
kwa umahiri mkubwa.
Mwandishi Wetu
No comments:
Post a Comment