VIDEO: Kutoka Ziara Maalum Mkoani Tabora: JPM kuendelea 'kuchuja vilaza wa upinzani'.. Bashe amuangukia aibane ACACIA.. #share..
RAIS John Magufuli amesema ataendelea kuteua viongozi kutoka vyama vya upinzani ili kuharakisha maendeleo ya Taifa na kwamba uteuzi wake hauangalii kabila wala dini.
Magufuli amesema hayo leo mkoani Tabora alipokuwa akihutubia wananchi katika siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu mkoani humo ambapo alizindua mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega, barabara ya Tabora-Nyaua na ile ya Tabora-Nzega.
Amesema katika Serikali yake viongozi wenye akili na weledi ni muhimu kwa ajili ya kujenga Tanzania yenye maendeleo hivyo ataendelea kuteua viongozi wenye weledi wa kufanya kazi katoka vyama pinzani.
Pia amesisitiza kuwa Tanzania sio nchi yenye ukabila kila mtu anahaki ya kuwa kiongozi hivyo hakuna ukabila wa aina yoyote .
Aidha Rais Magufuli amewataka wananchi wa Mkoa huo kuupisha mradi wa maji pindi utakapoanza kupita katika maeno hayo wasianze kudaifidia kwanza kwa kuwa mradi huo unatoka Mkoa wa Mwanza hivyo kufanya hivyo kutaweza kupunguza tatizo la maji katika eneo hilo.
"Ninawaomba wananchi wa tabora tuupitishe huu mradi wa maji kwa lengo la kuwasaidia watu wapate maji salama,ushirikiano ni muhimu ili kuendeleza mradi huu wa maji katika kuleta mabadiliko ya kweli,"alisema Magufuli.
Aidha Rais amesema miradi yote iliyoanzwa na marais wengine ataimalizia yeye na kuendeleza miradi mingine ili kujenga maendeleo kwa watanzania wetu.
=========≠=====Nae. MBUNGE wa Nzega mjini (CCM), Hussein Bashe amemwomba Rais John Magufuli kuendelea kuzibana kampuni za uchimbaji madini na ikiwamo Acacia akisema hiyo ni vita anayoiunga mkono kwani kampuni hizo zimeumiza wananchi kwa miaka mingi na kuwaacha na kilio.
Aidha Bashe amemshauri Rais Magufuli kumwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuinyima kampuni ya Resolute iliyokuwa ikioendesha mgodi huo mkoani Tabora isipewe marejesho ya kodi hadi itakapolipa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Sh bilioni 10 za kodi ilizotakiwa kulipa kwa uchimbaji madini.
Akizungumza mbele ya Rais Magufuli aliyekuwa katika ziara mkoani humo jana, Bashe alisema hatua ya kiongozi huyo mkuu wa Taifa kuzuia usafirishaji makanikia ya dhahabu kwenda nje ya nchi inasumbua Kampuni ya Acacia ambayo siku tano zilizopita ilitangaza kutolipa gawio kwa wanahisa wake kutokana na kuzuiwa usafirishaji wa makanikia kutoka Tanzania.
“Juzi Rais wa Acacia alitangaza kampuni hiyo haitalipa gawio kwa wanahiza wake kutokana na wewe kuzuia usafirishaji wa makontena ya mchanga wa dhahabu. Kama mchanga huo una kiwango kidogo cha madini kwa nini wamesema hawalipi gawio,” alisema Bashe huku akieleza anaunga mkono juhudi za Rais Magufuli kupambana na wizi wa rasilimali.
Gazeti la The Telegraph la Uingereza juzi lilimkariri Mtendaji Mkuu wa Acacia, Brad Gordon akieleza kwamba katika miezi sita iliyopita hadi Juni mwaka huu hisa za kampuni hiyo zimeporomoka kwa asilimia 29.
“Akiba yetu ya fedha imeporomoka kutoka Dola za marekani 318 hadi 176 katika kipindi hicho. Faida iliendelea kupatikana ingawa kwa asilimia mbili ambapo kabla ya kodi tulipata Dola milioni 99.5 lakini kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2,000 hatutalipa gawio,” alisema Gordon.
Katika maelezo yake, Bashe ambaye mara kadhaa amekuwa akiibana Serikali bungeni alisema kampuni hiyo ilipe fedha hizo kabla ya wao kudai fedha zao...
Fuatilia Hotuba ya Rais na Majibu kwa Mhe. Bashe..
Na: Jemah Makamba na Dalila Sharrif
No comments:
Post a Comment