Breaking News ! Baada ya Fununu ya kukamatwa, hatimae Lissu anasa mikononi mwa Polisi

Mbunge wa Singida Mashariki, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha CHADEMA Mheshimiwa Tundu Lissu, amekamatwa jioni hii akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa DAR akielekea Kigali kwenye mkutano wa marais wa vyama vya mawakili Afrika mashariki.


Amefuatwa na na Askari kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO) na Kumwambia aelekee Kituo cha Polisi cha kati kwa Mahojiano.
Akithibitisha taarifa hizi, afisa mwandamizi Chadema Makao makuu Tumaini Makene alisema.. 
Ni kweli. Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama wa Chama, Mhe. Tundu Lissu amekamatwa na polisi akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA) akiwa safarini kuelekea Kigali, Rwanda,  kushiriki Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki.

Tunafuatilia kwa ukaribu kupata details za sababu za kukamatwa kwake na kituo gani hasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.
*Makene

Awali Lissu alituma ujumbe huu kuashiria kuwa hali haikuwa shwari.. 

Council members. I'm at the airport getting ready to fly to Kigali for the EALS Governing Council meeting slated for tomorrow.

Persons introducing themselves as police officers from ZCO's office in Dar have come to arrest me and are taking me to the Central Police Station for interrogation.

Please notify everyone concerned.


About Author Matukio360

Matukio360 ni sehemu pekee inayokuletea matukio ya moto moto kutoka pande zote za dunia katika wakati ule ule yalipotokea yaani mubashara. Habari ni za uhakika na zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na kuandikwa kwa ueledi mkubwa na sio ukanjanja. Usibanduke katika ukurasa huu wa Matukio360, wajulishe na marafiki zako sasa wajipatie habari za uhakika.

No comments:

Post a Comment

Leo leo Plus

Start typing and press Enter to search