Exclussive ya Giggy Money na Bosi wa WCB: "Subirini muone matokeo.." #share
Chipukizi anaepasua anga za Bongo na medani za starehe za Dar, Gigy Money.. amezidi kufunguka na kuonyesha kutekwa kwake kihisia na kiranja wa bongo fleva ambae pia ni bosi wa lebo ya Wasafi "WCB" Nassib Abdull ‘Diamond Platnumz’..
Akinukuliwa 'kwenye maongezi 'na mtandao wa Jamboleo online, Giggy alitonya.. 'mahesabu yote yamekamilika na ninachokifanya kwa sasa ni kuweka sawa mtego kwa kumnasa rasmi...'
Katika siku za karibuni katika mitandao ya kijamii kumeonekana kusambaa kwa kasi kubwa kwa picha zinamuonesha Gigy Money akiwa na Diamond wakiwa kwenye mandhari tofauti-tofauti.
![]() |
Giggy hapa akiwa sambamba na Rich Mavoko enzi zileee !! |
Katika siku za karibuni katika mitandao ya kijamii kumeonekana kusambaa kwa kasi kubwa kwa picha zinamuonesha Gigy Money akiwa na Diamond wakiwa kwenye mandhari tofauti-tofauti.
Gigy amesisitiza katika safari yake ya kumnasa Chibu yuko ‘serious’ kabisa na kawaida kumpenda mtu akikubali kuwa mateka basi anatekwa. “Wangapi wanaonekana kama washapita tu, yeye mwenyewe mbona yupo tayari sema ntakuwa kama natoa siri,”.
No comments:
Post a Comment